Wakuu wa Mikoa wote nchini wametakiwa kufika kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kwa ajili ya kutoa taarifa ya ugawaji wa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo baada ya kukabidhiwa Desemba 10 mwaka uliopita

Wito huo umetolewa Jijini Dodoma na Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo ambapo amesema kuwa Wakuu wa Mikoa wote wametakiwa kuwa jijini Dar es Salaam kesho jumatatu kujieleza kwa Rais John Magufuli kuhusu vitambulisho walivyopewa kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo.

“tumewaandikia barua wakuu wa mikoa watoe maelezo juu ya ugawaji vitambulisho, namna lilivyofanyika. Lakini majibu watawasilisha wenyewe mbele ya Rais. Katika suala la vitambulisho kuna mikoa bado imegawa kwa asilimia mbili na nne wakati wengine wameshafika zaidi ya asilimia 94. Lazima tukazungumze na kujua changamoto ni nini na tunatokaje,,”amesema Jafo

 

Mnyeti aruhusu wanaApolo kuingia bure kwenye ukuta wa JPM
TAWIA wamuomba JPM kuanzisha wizara ya wajane