Mchambuzi wa masuala ya Kisiasa na mdadisi wa masuala ya Kiuchumi, Majid Mjengwa amesema mtu mwenye kuelewa anaweza akawaelewesha watu 1,000 na mwerevu mmoja anaweza kuwapotosha watu 1,000 akiamua.
Mjengwa ametoa sentensi hiyo wakati akifanya mahojiano na Dar24 Media kuhusu utata wa suala la mkataba wa uendelezaji wa Bandari kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai na kusema “kwahiyo basi mtu mjinga mmoja anaweza kuwa na kazi kubwa sana ya kuwapotosha werevu watatu.”
Amesema, “Bandari ni ushindani sisi hatuna bandari peke yetu –Mjengwa, kwa mujibu wa takwimu za kimataifa Container Port Perfomance Index (CPPI) ya mwaka 2022 inasema kwamba Tanzania ni ya 312 duniani kati ya 348”
Aidha ameongeza kuwa, “Kauli za watu wanaoaminiwa kwenye jamii zitatengeneza hofu –Mjengwa, lazima Tuseme hili Mjengwa.