Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Nigeria kwa wiki mbili, wamekuwa wakikusanya mapendekezo ya kubadili Katiba ambapo mmoja wa raia amependekeza kubadili jina la nchi hiyo kuwa United African Republic (Jamhuri ya Muungano Afrika).

Aliyependekeza wazo hilo ni Adeleye Jokotoye ambaye  ni mshauri wa masuala ya kodi katiaka jiji la Lagos, amesema kubadili jina ni ishara wa mwanzo mpya ikienda sambamba na kubadili katiba ya nchi hiyo.

Jina Nigeria lilipendekezwa mwishoni mwa karne ya 19 na mwandishi wa habari wa Uingereza, Flora Shaw, ambaye baadaye aliolewa na msimamizi wa kikoloni, Bwana Frederick Lugard.

Nigeria limetokana na mto Niger, unaingia kutoka  Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo na kuingia kwenye bahari ya Atlantiki.

Pendekezo hilo la kubadili jina limewaganya wananchi na viongozi wa taifa kwenye mitandao ya kijamii kwenye taifa   hilo  linaloongoza kwa wingi wa watu kwenye bara la Afrika ikikadiriwa kuwa na watu zaidi ya mil. 200.

Sabaya, walinzi wake walivyopandishwa kizimbani leo
Rais Karia asema alivyoisaidia Young Africans