Chakula tunachokula kina mchango mkubwa katika kuongeza mbegu za kiume, vyakula vingi vya kisasa havina uwezo wa kuongeza uwingi wa mbegu za kiume.

Inashauriwa kupunguza matumizi ya sukari na vyakula vya ngano na kuongeza zaidi ulaji wa matunda, mboga za majani na mafuta yenye afya.

Chini hapa ni baadhi ya vyakula vinavyochagiza uzalishaji wa mbegu za kiume kwa wingi, kwa mujibu wa makala mbalimbali za afya zimefanyia utafiti vyakula hivi na kugundua mchango mkubwa katika kuongeza uzalishaji wa mbegu za kiume kwa mwanaume kama ifuatavyo.

Matumizi ya kitunguu swaumu.

Kitunguu swaumu kina Selenium ambayo husaidia kuongeza spidi ya mbegu na pia huondoa sumu. Vile vile Kitunguu swaumu kina ‘Allicin’ ambayo huongeza msukumo wa damu kwenda kwenye uume.

Hivyo basi ni vyema kuongeza ulaji wa kitunguu swaumu kwenye chakula unachopika ambapo unaweza kutafuna punje 2 au 3 kila unapoenda kulala au unaweza kukatakata hizo punje 3 vipande vidogo vido (chop) kisha unywe na maji.

Usile zaidi ya punje 3 kwa siku.

Matumizi ya Mayai

Mayai yanachukuliwa kama mbadala wa uhakika zaidi katika kuongeza uwingi wa mbegu pamoja na kuongeza spidi au kasi yake. Yana vitamini E nyingi na protini ya kutosha vitu viwili mhimu katika kuongeza mbegu. Tumia mayai ya kienyeji zaidi na sio ya kisasa.

Ndizi

Ndizi zina Magnesiamu, Vitamini B1 na Vitamini C, vitu ambavyo ni mhimu sana kwa ajili ya kutengeneza mbegu za kiume. Vile vile Ndizi zina kimeng’enya kimoja adimu sana kijulikanacho kama ‘Bromeliad’ ambacho husaidia kuziweka sawa homoni zinazohusiana na tendo la ndoa.

Matumizi mbegu za maboga

Mbegu za maboga zina kiasi kingi cha madini ya Zinki ambayo ni muhimu katika kuundwa au kutengenezwa kwa mbegu za kiume na homoni ya testosterone.

Vile vile mbegu hizi zina vitamini B, C, D, E, na K ambazo zote ni vitamini mhimu katika kuongeza hamu ya kushiriki tendo la ndoa na nguvu kwa ujumla.

Kunywa maji mengi kila siku
Kutokunywa maji ya kutosha kila siku kuna uhusiano wa moja kwa moja na kupungua kwa uwingi wa mbegu. Mbegu zako zimetengenezwa kwa maji, zipo kwenye hali ya kimiminika hivyo maji ya kutosha husaidia kutengenezwa kwa mbegu nyingi Kutegemea na uzito wako unaweza kuhitaji maji lita 2 mpaka 3 kila siku.

Tumia vyakula vyenye folic asidi kwa wingi
Vyakula hivi ni pamoja na tunda la parachichi na karoti, mbegu za maboga, ufuta, alizeti, maharage, chungwa, papai na bamia.

Johari kuzindua filamu siku ya Idi Mosi Mbeya
Video: Kutupa mifuko ya plastiki faini Sh milioni 5, Mwalimu matatani kwa kumpofua Mwanafunzi