Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye amekiri kuwepo kwa udhaifu katika sheria ambazo zinaliongoza Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) lililopewa dhamana ya kusimamia na kustawisha shughuli za sanaa nchini.

waziri Nape amedai kwa sasa baraza hilo linakutana na wasanii wakati wa kuzifungia kazi zao pale wanapokiuka maadili ya kazi za sanaa.

“BASATA ambalo ndio baraza lipo chini yangu sio rafiki kwa msanii,” Waziri Nape alikiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM. “Msanii anakutana na BASATA unapotakiwa kufungiwa wimbo wake au anapotakiwa kuonywa kwa kupewa adhabu. Nataka sheria ilifikishe sehemu BASATA awe mlezi wa msanii. Sasa hivi wakiamua kuwa walezi akina Mngereza na wenzake ni kwa mapenzi yao. Lakini nataka sheria iwalazishe wao sio polisi, wao ni wazazi wanaotakiwa kulea na kuendeleza,”

Aliongeza, “Hata Bodi ya filamu wasionekane tu wakati wakufungiana, waonekane pia wakati msanii anaanza kukua mpaka anafika mbali zaidi. Kwa hiyo changamoto kubwa kwetu mfumo sio rafiki wa kuifanya sanaa yetu itoke hapa iende mbele,”

Waziri huyo amesema serikali ikirekebisha sheria za sanaa na kuwa rafiki kwa watumiaji anaamini sekta ya sanaa inaweza kutoa mchango mkubwa katika kukuza pato la Taifa.

Harmonize afunguka juu ya ushindani ndani ya WCB
Wastara aaga mwaka na ujumbe mzito '' hakuna kitu kibaya kama kupoteza furaha na tumaini''