Mwandishi mahiri wa vitabu nchini Tanzania Yericko Yohanesy Nyerere amefanikiwa kupeperusha vyema bendera ya Tanzania baada ya kunyakua tuzo ya Mwandishi Bora wa Vitabu Barani Afrika kwenye tuzo za ZIKOMO AFRIKA zilizotolewa Novemba 18,2023 nchini Zambia

Nguli huyo amesheherekea ushindi wake kwa kuchapisha jumbe mbalimbali kwenye mitandao yake ya kijamii akiwashukuru wale waliompigia kura na kufanikisha ushindi huo pamoja na kutangaza ofa maalum ya punguzo kubwa kwenye bei za vitabu vyake vya UJASUSI.

Hata hivyo Nyerere hakuacha pia kuishukuru mizimu kwa kuchapisha ujumbe uliosomeka ”Idumu Mizimu”

Yericko Nyerere ni mdau mkubwa wa Dar24 Media na mara kadhaa ameshiriki kwenye kipindi cha MAELEZO kufafanua masuala mbalimbali ya Kijasusi yanayopatikana kwenye vitabu vyake alivyowahi kuvichapisha.

Jumla ya Watanzania 13 walifanikiwa kushinda tuzo za ZIKOMO AFRIKA AWARDS 2023 kwenye vipengere mbalimbali.

Tuzo hizo hutolewa kila mwaka kwa watu mashuhuri waliofanya vizuri katika sekta mbalimbali kama vile Sanaa, Masuala ya Kijamii, Uandishi wa Habari, Ujasiriamali na masuala mbalimbali ya kijamii

Gesi: TPDC iandae mpango wa muda mrefu - Dkt. Biteko
Wakurugenzi wawili watimuliwa kazini