Wakurugenzi wawili wa halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani na Halmashauri ya Mji wa Ifakara mkoani Morogoro wamesimamishwa kazi kuanzia ili kupisha ichunguzi.

Hayo yamejiri baada ya waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa kupokea taarifa ya awali ya timu iliyoundwa kuchunguza tuhuma za wakurugenzi hao kushindwa kusimamia miradi ya maendeleo katika halmashauri zao kwa nyakati tofauti.

Wakurugenzi hao ni, Butamo Nuru Ndalahwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara mkoani Morogoro, Lena Martin Nkaya.

Timu hiyo iliyoundwa na Katibu Mkuu kwa maelekezo ya Waziri Mchengerwa imebaini mapungufu ikiwemo kushindwa kusimamia miradi ya maendeleo.

Uamuzi huo wa kuwasimamisha kazi umezingatia Kanuni ya 37 (1) na 38 (1) ya Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2022 ili kupisha uchunguzi wa kina.

Aidha amewasisitiza Wakurugenzi wote wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kutekeleza majukumu yao kikamilifu ikiwa ni pamoja na kusimamia miradi ya maendeleo.

Mchengerwa ameendelea kusisitiza kuwa hatasita kuchukua hatua stahiki kwa atakayethibitika kutenda kinyume.

Nyerere aishukuru Mizimu ushindi tuzo ya mwandishi bora wa vitabu Afrika
Wizara ya Madini kushiriki jukwaa la biashara, Diaspora kutoa maoni