Mbunge wa jimbo la Simanjiro James Ole Milya amewataka vijana wa Baraza la Vijana Chadema kutumia muda vizuri kujiandaa kuwa viongozi wazuri na wa mfano wa  kuigwa kwa kutumia muda walionao Vizuri.

Leo jijini Dar es salaam akizungumza na vijana hao Mh. Ole milya amewaambia vijana hao wasipoteze muda kwa mambo yasiyo na msingi  bali kujikita zaidi  katika kuhakikisha wanatengeneza mazingira ya kuwa viongozi kama Nkwame Nkuruma,Mwl Nyerere Nelson Mandela na wengineo waliopigania nchi zao na ukombozi wa Afrika.

”Ni muda wa kujiandaa  na kuwa viogozi vijana wa mfano kama walivyokuwa wakina Mwl Nyerere, mandela, na wengine hawakupoteza muda na sasa tunawasoma kama vijana waliopambana kwa ajili ya mataifa yao”.- Ole Milya.

Aidha Mbunge huyo amewataka vijana hao kuwa mstari wa mbele kuhakikisha ya kuwa hakuna mwananchi anayeonewa huku wakitakiwa kuzingatia sheria za nchi.

Ole Milya amewaambia pia vijana hao watambue kuwa kwa sasa bunge halipo huru hivyo vijana wanapaswa kuamka na kupambana na hali hii inayoendelea nchini kwa kupaza sauti za kutokubaliana na kinachoendelea bungeni.

 

 

Ripoti Ya Utafiti Utumikishwaji Watoto Yazinduliwa
Lowassa: Uteuzi wa Rais Magufuli Uzingatie makundi yote ya Vijana Bila Itikadi ya Vyama