Bifu jipya limeibuka katika tasnia ya Bongo Flava kati ya rapa Nay wa Mitego na Ommy Dimpoz baada ya wimbo mpya wa ‘Shika Adabu Yako’ wa Nay kuanza kuyasoma masafa ya redio.

Nay wa Mitego

Katika wimbo huo, Nay anawashambulia wasanii wengi na kumtaja Ommy Dimpoz akidai mtaani kuna tetesi kuwa ‘jogoo hawiki’.

“Huyu jamaa anajiita Dimpoz, Pose kwa Pose, wanae wanalalamika hawamjui shemeji, mtaani kuna tetesi mwana hapigi mechi, mara oh jogoo hawiki, huwa hawaoneshi shemeji,” anarap Nay wa Mitego kwenye Shika Adabu Yako.

Ommy amevunja ukimya kwa kupost video fupi ya mrembo na kujibu mashambulizi ya Nay wa Mitego.

Barua ya wazi kwa Neema wa Mitego kwanza pole kwa Malezi ya Watoto ambao mama zao wamekukimbia, hakuna Mwanamke ambae anaweza kuishi na mwanaume mwenye tabia za kike kama zako ? inatakiwa ujiulize una tatizo gani maana km umaarufu mavi unao,nyumba unayo,magari unayo na hivyo ndo vitu dada zetu wanapenda lakini kwanini wanakukimbia pili kila nikiwaangalia watoto naona kabisa hamjafanana kuna umuhimu wa DNA Da Neema trust me. Hiyo video nimekuwekea hapo juu ni kukuonyesha kuwa mimi na wewe Ligi zetu hazifanani ? vitu navyokula mimi wewe utaishia kuviona kwenye TV maana kuvipata mpaka uwe Unapanda sana Ndege sasa mimi najaza passport ya Tatu wakati wewe hata kurasa 4 za passport yako ya kwanza hujamaliza ? Sasa wewe ushazoea wanawake zako wa jumuiya basi unataka kila mtu apost demu wake haya sasa Chuma hiko kimetoka ulaya kuja kufuata dodoki ??nimekujibu ili nikusaidie promo ya nyimbo yako Atleast upige na Vishoo baba ?? Sema nakuomba usirushe ngumi tu maana nakujua Mzee wa Kupanic Maana katika hao mabebi mama wako kuna mmoja nilishapitaga nae Uliza vizuri atakwambia kama jogoo anawika au vipi ?Ukitaka kudownload wimbo wa @naytrueboy #ShikaAdabuYako nenda kwenye bio ya Da Neema ?

A video posted by SnapChat ommydimpoz (@ommydimpoz) on

Angalia Orodha Ya Mabondia 10 Bora Kwa Nyakati Zote
Mabingwa Wa Africa Wakabidhiwa Zawadi Nono