Serikali ya nchi ya Marekani, inajitayarisha kwa ongezeko la wahamiaji wanaojaribu kuvuka mpaka upande wa kusini mwa taifa hilo.
Hatua hiyo, inakuja kufuatia kumalizika kwa Title 42 sera ambayo inahusishwa na janga iliyoiruhusu Marekani kuwafukuza wahamiaji zaidi ya milioni 2.8.
White House, ambayo inalaumiwa kwa picha za vurugu kwenye mpaka, inajitetea dhidi ya ukosoaji na kusema Bunge linahitaji kuchukua hatua.
Aidha, ofisi hiyo inasema ilifanyakazi kushughulikia wasi wasi kwamba matukio kama hayo huenda yakawa ni kawaida kwenye mpaka wa kusini wakati Title 42 itakapoondolewa.
Afisa wa ngazi ya juu wa uhamiaji wa Rais, Joe Biden alitangaza kanuni mpya inayohusu wahamiaji ambao wanavuka mpaka kuwa wataondolewa na hawastahili kupewa hifadhi, isipokuwa kupitia app ya CBPone ambayo itaendelea kutoa ulinzi kwa waomba hifadhi.