Jumla ya watu 37 wameuawa nchini Thailand, kufuatia mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Panya Kamrab kuwafyatulia risasi, huku 24 kati yao wakiwa ni watoto, kitendo kilichoibua simanzi miongoni mwa raia wengi wa nchi hiyo na kwingineko Ulimwenguni.

Tukio hilo, limetokea katika kituo cha kulea watoto, kilichopo katika Mkoa wa Nong Bua Lamphu, ambapo mtu huyo aliyekuwa akijihami akiwa na kisu na Bunduki kujipiga risasi baada ya kuhakikisha amefanya mauaji hayo na kumuuwa mkewe na mwanawe waliokutwa wamekufa.

Polisi imesema, mshambuliaji huyo Panya Kamrab (34), alikuwa ni afisa wa zamani wa polisi ambaye alifutwa kazi mwezi Juni kwa kupatikana na dawa za kusisimua aina ya methamphetamine.

Mauaji hayo, yanatajwa kuwa mbaya zaidi katika historia ya Thailand na kwamba idadi ya vifo vya matukio ya ufyatuaji risasi shuleni yanafanana na yale ya nchini Marekani.

Hata hivyo, hatua hii inakuja ikiwa miaka miwili baada ya mwanajeshi mmoja kuua watu 29 katika shambulio la halaiki katika maduka makubwa ya Thai na kambi ya jeshi, huku shambulio hilo likichochea ulinzi binafsi wa kulinda uhai kwa wananchi wa taifa hilo.

Kiwango cha mauaji ya bunduki nchini Thailand, ingawa ni cha chini kuliko kile cha Marekani lakini ni cha juu zaidi barani Asia ambapo hata hivyo mazoezi ya ufyatuaji risasi yamekuwa si sehemu ya utamaduni kwa nchi hiyo ambayo madaraja ya kijeshi yameenea kuanzia shule na ofisi, huku huduma za afya ya akili zikiwa ni chache.

Kenya na Ethiopia zajadili uhusiano wao kiuchumi
Ibenge: Nina mbinu za kutupeleka MAKUNDI