Basi la abiria maarufu kama daladala linalofanya safari zake jijini Dar es Salaam, limeacha njia na kuingia kwenye njia barabara maalum ya mabasi ya mwendo kasi na kuligonga basi moja la mwendo kasi.

Picha za tukio hilo zinaonesha daladala hiyo ikiwa iimevuka kizuizi cha barabara kinachotenganisha kati ya barabara ya kawaida na ile ya mwendo kasi na kulibamiza ubavuni basi hilo.

Hata hivyo, bado Mamlaka zinazohusika hazijatoa taarifa rasmi kuhusu tukio hilo ikiwa ni pamoja chanzo cha ajali hiyo na madhara yake.

Guus Hiddink Afichua Siri Ya Kuikataa Leicester City
Forbes wataja wana hip hop matajiri zaidi duniani, Drake achomoza