‘Vitita’ vya fedha taslimu vimekutwa vikiwa kwenye mabegi na magunia ndani ya nyumba ya aliyekuwa Rais wa Sudan, Omar al-Bashir baada ya Baraza la Usalama la Kijeshi kufanya upekuzi kwenye makazi yake.
Kwa mujibu wa ripoti, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Sudan imeeleza kuwa imeanzisha uchunguzi wa kina ili kumfungulia mashtaka ya uhujumu uchumi.
Kwa mujibu wa BBC, vyombo vya usalama vimekuta vitita vya Dola za Kimarekani, euros, Pounds na fedha za Sudan ambazo kwa jumla ni zaidi ya $130 milioni.
Chanzo cha kuaminika kimekaririwa na Reuters kikieleza kuwa mabegi na magunia yenye fedha yamekutwa ndani ya nyumba ya kiongozi huyo, ambayo ni zaidi ya $351,000, €6m ($6.7m; £5.2m) na Bilioni tano za Sudan ambazo ni sawa na $105m.
#Sudan authorities seize Al #Bashir cash stash #bashirhasfallen #SudanNews #SudanProtests #SudanUprising #Sudan_Revolts #Sudan_UpRising https://t.co/sup6OnZ9TP pic.twitter.com/oPID9FZNhI
— Radio Dabanga (@Radiodabanga) April 19, 2019
Al-Bashir ambaye aliiongoza nchi hiyo kwa kipindi cha miaka 30, alikamatwa kufuatia maandamano makubwa ya kupinga utawala wake, aliwekwa kwenye kifungo cha ndani na kisha kuhamishiwa kwenye gereza lenye ulinzi mkali la Kobar.
Mwendesha mashtaka amesema kuwa watakwenda ndani ya gereza hilo kwa ajili ya kumhoji.