Siku mbili baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuagiza kila mkazi wa mkoa huo anaemiliki silaha ya moto kuiwasilisha kwa ajili ya ukaguzi, Rais John Magufuli amekuwa mwananchi wa kwanza kutekeleza agizo hilo.

Rais Magufuli ambaye makazi yake ni Ikulu iliyoko Magogoni jijini Dar es Salaam, leo amewasilisha silaha yake chini ya uangalizi wa Kamanda wa  Jeshi la Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro.

Magufuli awasilisha Silaha 2

Picha kutoka ikulu zinamuonesha Rais Magufuli akiwa anakabidhi bastola pamoja na bunduki moja kubwa.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliagiza wananchi wote wanaomiliki silaha zao kihalali kuziwasilisha kwa ajili ya ukaguzi lakini pia kwa wale wanaozimiliki kinyume cha sheria waziwasilishe pia na watapewa kitita cha shilingi milioni moja kwa kila silaha.

Assah Mwambene ang'olewa Idara ya Habari Maelezo
Kipre Tchetche Aweka Rekodi CAF