Kikosi cha Simba SC kimerejea jijini Dar es salaam mapema leo Alhamis (Novemba 10) majira ya asubuhi kikitokea mkoani Singida kupitia Dodoma.

Simba SC ilikua Singida kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa jana katika Uwanja wa Liti dhidi ya wenyeji Singida Big Stars iliyokubali kutoa sare ya 1-1.

Kikosi cha Simba SC kimewasili Dar es salaam kwa Ndege ya Shirika la Ndege ya Tanzania, na moja kwa moja kimeelekea kambini kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ihefu FC utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Jumamosi (Novemba 12).

Matokeo ya jana dhidi ya Singida Big Stars yameifanya Simba SC kufikisha alama 18 ikishika nafasi ya tatu, ikitanguliwa na Azam FC na Young Africans zenye alama 20 kila mmoja.

Ihefu FC itakayocheza na Simba SC Jumamosi (Novemba 12) ipo mkiani mwa msimamo wa wa Ligi Kuu, ikiwa na alama tano baada ya kucheza michezo tisa.

Peter Banda kuikosa Ihefu FC
Mo Dewji, Ahmed Ally waipongeza Young Africans