Leo Machi 24, 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewaapisha Mabalozi na Mawaziri aliowateua hivi karibuni, ambapo kati ya Mawaziri hao ni Waziri mpya wa Habari, Sanaa, Burudani na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ambaye mara baada ya kula kiapo amefika na kupokelewa na Wafanyakazi wa wizara yake katika ofisi za Wizara hiyo jijini Dar es salam.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akipokelewa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Annastazia James Wambura katika Ofisi za Idara ya Habari – MAELEZO mara baada ya kutoka kula kiapo leo Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akipokea shada la maua kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa Wizara hiyo Bi. Flora Mwnyenyembegu wakati wa mapokezi ya Waziri huyo yaliyofanyika katika Ofisi za Idara ya Habari – MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Annastazia James Wambura(wapili kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi. Nuru Khalfan Milao wakati wa mapokezi ya Waziri huyo yaliyofanyika katika Ofisi za Idara ya Habari – MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akipokelewaakiweka saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kupokelewa na watendaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Taasisi zake mapokezi yaliyofanyika katika Ofisi za Idara ya Habari – MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Annastazia James Wambura

Magazeti ya Tanzania leo Machi 25, 2017
Wapiga chapa watakiwa kujisajili