Picha ya wachezaji wa timu ya taifa ya vijana ya Ujerumani imeleta utata miongoni mwa wanajamii, baada ya kuwekwa katika mitandao ya kijamii, kwa kutafsriwa kama ubaguzi wa rangi dhidi ya waafrika.

Picha hiyo inawaonyesha wachezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani, wakiwa wamepakwa rangi nyeusi.

Deinster SV wamekuwa wa kwanza kuiweka picha hiyo katika mtandao wa kijamii wa Facebook na imeleta tafrani kwa kila aliyeiona na kuacha ujumbe ambao ulihushwa na ubaguzi wa rangi.

Hata hivyo ujumbe uliokua umeandikwa katika picha hiyo ulilenga kuwasisitiza kuachwa kwa tabia za kuwabagua wakimbizi ambao wamekua wakiingia kwa wingi katika mataifa ya barani Ulaya.

Ujumbe wa picha hiyo umesomeka hivi: “”Ghasia dhidi ya wakimbizi ni dhaifu tu. Emad na Amar, wewe ni mmoja wetu kama kila mtu mwingine na sisi ni furaha wewe ni pamoja na sisi. ”

Baada ya picha na ujumbe huo kuwekwa katika mtandao wa kijamii, dakika kadhaa baadae umeeonekana kusambaa kwa watumiaji wengine wa mtandao huo zaidi ya 2,000.

Wengine wamekwenda mbali zaidi kwa kuupeleka katika mtandao wa Twitter na mmoja kati yao ameandika: “Ninaelewa ishara hii, lakini haukupaswa kuwa katika mtazamo wa rangi nyeusi.”

The original team photo for lower league side Picha Halisi

Kutokana na ujumbe kuendelea kusambaa, kocha mkuu wa timu ya taifa ya vijana ya Ujerumani Soenke Kreibich, alilazimika kutoa ufafanuzi wa picha hiyo kwa kusema wametafsiriwa vibaya na hawakuwa na dhamira iliyoelezwa katika mitandao ya kijamii.

Amesema walipiga picha ya pamoja ya wachezaji wote na walikua katika hali ya kawaida, lakini cha kushangaza, baadhi ya watu wameichukua na kuiwekea rangi na kuianika katika mitandao ya kijamii, tena kwa kuiwekea ujumbe tofauti.

Picha ya kwanza iliyowekwa katika mtandao kijamii wa Facebook ilipata like 17,000, kitendo ambacho kimetafsriwa kama kuwapendeza baadhi ya watu.

Ferguson: Ni Ndoto Kwa Man City Kucheza Kama FC Barcelona
Aston Villa Wamshimamisha Gabriel Agbonlahor