Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe ameachana rasmi na ukapela na kuanza maisha ya ndoa, baada ya kufunga ndoa jana na mrembo aliyemvisha pete ya uchumba mwezi Mei mwaka huu, Anna Mtura.

Wawili hao walizama katika visiwa vya Zanzibar na kula kiapo cha kuwa mwili mmoja, kuishi pamoja kwenye shida na raha, uzima na maradhi.

Zitto ndoa 2

Anna Mtura aliwahi kuwa mfanyakazi wa gazeti la The Guardian lakini aliachana na kazi hiyo muda mfupi baada ya kuvishwa pete ya uchumba na mwanasiasa huyo machachari.

Dar24 inawatakia kila la kheri na inawapongeza kwa hatua hiyo kubwa maishani.

 

Sitta ahamishwa nyumba ya Serikali, Msako nyumba kwa nyumba waja Dar
Ugaidi: Watu 80 wauawa kwa risasi wakisherehekea Ufaransa