Gavana wa Jimbo la Jos, Nigeria Simon Lalong, ameahidi zawadi nono kwa wachezaji wa Palteau United, kuelekea mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Simba SC, utakaochezwa keshokutwa Ijumaa, Novemba 27.

Lalong, ametoa ahadi hiyo alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye kambi ya timu ya Plateau United, ambapo amewataka wachezaji kupambana na kuifunga Simba SC kwenye mchezo huo.

Kiongozi huyo ameahidi zawadi ya Naira Milioni 1 sawa na dola za kimarekani 2,600 kwa kila mchezaji. Pia ameiahidi zawadi ya jumla ya basi la siti 32 ambalo litakua mali ya klabu ya Plateau United, ambayo inashiriki kwa mara ya kwanza Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Msafara wa Simba SC wenye watu 40, ulitarajiwa kuwasili mjini Lagos, Nigeria leo mchana wakitokea Addis Ababa-Ethiopia, baada ya kuondoka nchini jana jioni na ndege ya Shirika la ndege la Ethiopia.

TAKUKURU kuchunguza ubadhirifu wa fedha CAF
Kocha Kaze aahidi soka safi Azam Complex

Comments

comments