Mahakama nchini Kenya, imemhukumu kifo aliyekuwa afisa wa Polisi, Fredrick Leliman, aliyepatikana na hatia ya kuhusika na wakili maarufu wa haki za binadamu Willie Kimani mwezi Juni mwaka 2016.

Wakili huyo, pamoja na mteja wake Josephat Mwenda, na dereva wake wa texi Joseph Muiruri waliuawa na miili yao kupatikana katika mto ulio nje kidogo ya jiji la Nairobi, wiki mbili baada ya kutoweka.

Jaji, Jessie Lessit amesema Leliman alibainika kuhusika na mpango wa kumteka na kumuua, wakili huyo, katika kesi ambayo imekuwa ikifuatiliwa kwa karibu nchini Kenya.

Polisi waliopatikana na hatia ya kumuua wakili wa haki za Binadamu nchini Kenya, Willie Kimani mwaka 2016. Picha ya ibtimes.

Mbali na Leliman, ambaye amekuwa mshukiwa mkuu Maafisa wengine wa zamani wa polisi Stephen Cheburet na Peter Ngugi, wamefungwa jela miaka 30 huku Sylvia Wanjiku akipewa hukumu ya miaka 24.

Wakili Kimani, alikuwa akimtetea Mwendwa ambaye ni mwendesha bodaboda, aliyemtuhumu Polisi Leliman, kwa kumpiga risasi bila kosa katika kituo cha ukaguzi mwaka 2015 na hivyo, alikuwa aKItafuta haki.

Hukumu hiyo, imetolewa wakati Polisi nchini Kenya, wakiendelea kukabiliwa na rekodi mbaya ya kutekeleza mauaji ya raia kiholela, na kuwateka washukiwa wa makosa mbalimbali.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Februari 5, 2023
Lissu: Risasi zimempa maisha Dereva wangu