Kocha Msaidizi wa Polisi Tanzania, John Tamba amesema kuwa wanaanza kufanya maandalizi kwa mchezo wao ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba SC utakaochezwa jijini Dar es salaam Mei 24.

Katika mchezo wao uliopita Polisi Tanzania ilipata ushindi dhidi ya Mtibwa Sugar kwa mabao 3-1 Uwanja wa Ushirika, Moshi mkoani Kilimanjaro.

Kocha Tamba amesema nguvu kubwa inaelekea katika mchezo dhidi ya Simba SC ili kupata ushindi ambao utakua na msaada mkubwa kwa kikosi chao ambacho kinapambana kujinusuru kushuka daraja msimu huu 2022/23.

“Tunaanza maandalizi kwa mchezo wetu dhidi ya Simba SC ambao utakuwa Mei 24, hautakuwa mchezo mwepesi lakini ni lazima tufanye jitihada kupata ushindi.

“Ni mechi ngumu itakuwa lakini tunaamini mechi zilizobaki ni muhimu kufanya kazi kubwa ambayo itatupa nguvu ya kubaki kwenye ligi tunaamini tutafanya kazi kubwa katika maandalizi ya mchezo wetu ujao,” amesema

Marcus Rashford apandisha mzuka Man Utd
Mshindi promosheni ya mazishi aingia mitini