Askari wa watatu wa Jeshi la Polisi wamefariki na wengine wawili wamejeruhiwa baada ya gari lao kupata ajali walipokuwa wakisindikiza msafara wa Rais John Magufuli kutoka Singida Kuelekea Dodoma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka aliwaambia waandishi wa habari kuwa ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 9 alasiri katika kijiji cha Isuna, Wilani Ikungi mkonai humo.

Alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni moja kati ya matairi ya gari walilokuwa wamepanda askari hao kupasuka hali iliyopelekea dereva kushindwa kulimudu gari hilo. na hatimaye kupinduka.

Rais John Magufuli alikuwa akitokea Mkoani Singida alipoenda kuhudhuria sherehe ya maadhimisho ya miaka 39 ya Chama Cha Mapinduzi.

Mazombi yadaiwa kushambulia na kujeruhi watu hovyo Zanzibar, Polisi wanena
Tetemeko kubwa la ardhi laleta maafa, laangusha jengo la ghorofa 17