Watu sita (06) wamefariki dunia na wengine wanne wamejeruhiwa katika ajali iliyo husisha gari Toyota Noah kugongana na lori aina ya scania katika eneo la ALKATANI kata ya Sepeko tarafa ya Kisongo wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha katika barabara ya Arusha Babati.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo ameseama ajali hiyo imetokea tarehe 19.04.2022 muda wa saa nne usiku na kuyataja magari hayo kuwani Toyota Noah yenye namba za usajili T.189DFY likitokea Arusha mjini kwenda Karatu na lori lenye na mbaza usajili T.250CAA ambapo lori hilo lilikuwa linatokea makuyuni kwenda Arusha mjini.

ACP Masejo amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe waderevaa ambapo alishindwa kulimudu gari hilo aina ya toyota Noah hiyo.

Kamanda Masejo amesema kuwa Jeshi hilo linamshikilia dereva wa roli aliyesababisha ajali hiyo.

Kamanda Masejo amesema kuwa bado wanaendelea kufanya uchunguzi kufamu majina halisi ya abiria waliofariki katika ajali hiyo na amewaomba wananchi kufika katika hosptali ya rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru kutambua mili ya marehemu.

ACP Masejoa metoa wito kwa watumiaji wa vyombo vya moto kuwa waangalifu wakati wa matumizi ya vyombo hivyo ilikupunguza ajali ambazo zinagharimu maisha ya watu.

Nilivyomnasua Mpenzi wangu kwenye Uraibu wa dawa za kulevya
Tuzo za Waandishi kutolewa Mei 3