Jeshi la Polisi nchini, limetoa taarifa ya ajali ya Bsi liendalo haraka ambayo ilitokea Februari 22, 2023 katika makutano ya barabara ya Morogoro na Jamhuri, Kisutu jijini Dar es salaam, huku likitoa wito kwa madereva kufuata na kuzingatia sheria na alama za barabarani ili kuepusha ajali.
Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi hilo iliyotolewa na Kamanda Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam, Muliro Jumanne imeeleza kuwa ajali hiyo ilihusisha Gari namba T122 DGW Aina ya Dragon mali ya kampuni ya UDART na gari ndogo yenye namba T978 DHZ aina ya Toyota Avanza Mali ya Rwanda Air.
UDART ilikuwa ikiendeshwa na dereva Shabani Ramadhani (43), akitokea Kivukoni kwenda Kimara na gari dogo lilikuwa likiendeshwa na Jumbe Mohamed (38) na ajali hiyo ilisababisha kugonga nyumba ya biashara wakati UDART ikijaribu kulikwepa gari dogo.
Taarifa hiyo imezidi kueleza kuwa, ajali hiyo ilisababisha baadhi ya abiria kupata majeraha madogo na walipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kuruhusiwa, huku watu wanne wakilazwa na kuendelea kupata matibabu katika Hospitali hiyo akiwemo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Ismail nimtembea kwa miguu.
Wengine ni dereva wa gari dogo, Jumbe Mohamed (38) Shukuru Omari (32) na Saidi Hasani (43) wote walikuwa ni abiria wa gari ndogo ambapo uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha jali ni uzembe na kutojali kwa alama za barabarani kwa dereva wa gari dogo kutochukua tahadhari.