Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya ndani, Charles Kitwanga amesema anamuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa MUNGU, kwani watu wanaomzunguka hawana nia njema, huku akimtaka kuwaangalia kwa makini na asiruhusu wamchafue.

Kitwanga ameyasema hayo wakati akiongea na Waandishi wa Habari nyumbani kwake na kuongeza kuwa mbali na kumuwekea vikwazo Rais pia kundi hilo limekuwa ni tishio kwa maslahi ya umma na likilenga kulinda maslahi binafsi.

Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya ndani, Charles Kitwanga.

Amesema, kundi hilo limejipenyeza katika kila sekta zikiwamo taasisi za umma na kuongeza kuwa ukiwa mkweli na una akili kuwazidi huwezi kufanikiwa kusonga mbele kwa lolote hadi uungane na genge hilo, linalomshauri rais ili kufanikisha masuala yao binafsi.

Hata hivyo, Kitwanga amesema ifikie hatua watu wafanye kazi na kusaidia Rais na si kufanya wizi wa fedha za watanzania akitolea mfanno kivuko kilichoharibika na kupeleka Kenya kwa matengenezo kuwa ni wizi mkubwa ambao unapaswa kupingwa kwa nguvu zote.

Mtandao mawasiliano Serikalini kuboreshwa
Polisi yatoa taarifa ajali ya Mwendokasi Kisutu