Jumla ya watuhumiwa 132 wamekamatwa na kufikishwa Mahakamani na Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga ndani ya mwezi mmoja (Machi 22 –  Aprili 26, 2023), ikiwa ni kati ya kesi 129 zilizoripotiwa na kufanyiwa kazi na kitengo cha upelelezi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoani Shinyanga, ACP. Janeth Magomi amesema hadi kufikia sasa ni kesi 62 zimesikilizwa zikiwemo za makosa ya ukatili wa kijinsia, kesi nne za mimba kwa Wanafunzi, mbili za ubakaji na moja ya kulawiti na watuhumiwa kufungwa kifungo cha nje na kulipa faini.

Amesema, ndani ya kipindi hicho pia Polisi  walifanikiwa kukamata Bunduki tano ambazo zilikuwa zikimilikiwa kinyume cha sheria aina ya Mark IV yenye namba TZCAR 89939 na risasi nne, Mark IV-K 9239 na risasi tatu, Mark IV – D 6,000 na risasi moja, Mark IV – MG 564884 na Short gun Birmingham England iliyokuwa na risasi moja.

Aidha, Kamanda Magomi amebainisha kuwa katika tukio jingine Polisi walifanikiwa kukamata vitu na vielelezo mbalimbali ikiwemo Pikipiki sita, Pombe ya Moshi lita 120, vifaa vya kupiga ramli chonganishi, Vipodozi vyenye viambata vya sumu ambavyo haviruhusiwi kwa matumizi ya binadamu, Pombe kali boksi 12 na vitu mbalimbali vilivyoibiwa madukani.

SIREFA: Singida tupo tayari kwa ASFC
Namungo FC yafunguka kushindwa Ligi Kuu