Mbunge wa Jimbo la Mikumi Joseph Haule, maarufu kama Professor Jay na mkongwe wa muziki wa HipHop hapa nchini ametoa neneo kwa wasanii wa HipHop wanaoshindwa kujiweka kibiashara ili kujiingizia kipato nje ya kazi wanazofanya.
Amesema wasanii wengi wa HopHop hawajiongezi kama wasanii wanaoimba na ndio maana wanakosa ‘dili’ mabalimbali ambozo zinawafaidisha wasanii wanoimba.
“Mtu anayeimba anapata ‘deal’ halafu mtu wa Hip Hop hapati na wapo kwenye nchi moja maana yake kuna mmoja anajiongeza na mwingine hajiongezi, kwa sababu hata haya makampuni na mikataba ya kibiashara hauwezi kuvipata kama umekaa nyumbani sebuleni wakuletee lazima uvihangaikie kuvipata, ni kwamba tumekuwa wazembe”, amesema Prof. Jay.
Ameongeza kuwa wsanii wa HipHop wanapata tabu kwa kuwa nyuma, anaamini wanafaida kubwa katika jamii kwa sababu wanaimba uhalisia wa maisha pia wanafanya vizuri kwenye matamasha kuliko wanoimba na hata mitaani wanakubalika.
Amemtaja msanii wa kike Maua Sama, ndiye anayestahili kuwa malkia wa Bongo kwa sababu anaijua historia yake tangu anahangaika kutoka kimuziki hadi sasa anavyoelekea kuwa shujaa.