Meneja wa klabu ya Newcastle United, Rafael “Rafa” Benítez Maudes ameungana na kiungo wa klabu hiyo Jonjo Shelvey kwa kutoa ahadi ya kuendelea kubakia klabuni hapo hata kama akishindwa kuinusuru isishuke daraja mwishoni mwa msimu huu.

Benitez, ambaye alikabidhiwa jukumu la kuhakikisha anainusuru Newcastle United miezi mwezi mmoja uliopita baada ya kutimuliwa kwa Steve McClaren, ametoa ahadi hiyo katika kipindi hiki ambacho anahimiza umoja na mshikamano kikosini mwake.

Benitez, mwenye umri wa miaka 55, amesema anaimani kwamba jukumu alilokabidhiwa ni zito na yeye alilikubali kwa kutambua ugumu wake, hivyo hana budi kupambana na kuamini atafautu.

Amesema ni vigumu kwa mtu kama yeye kukubali kuiopokea kazi nzito kama aliyokutana nayo klabuni hapo, lakini kutokanana mapenzi yake na mchezo wa soka alifanya maamuzi ili auonyeshe umma wa mashabiki namna anavyoweza kupambana.

Hata hivyo meneja huyo kutoka nchini Hispania, amedai kwamba endapo kikosi cha Newcastle Utd kitashindwa mtihani wa kubaki ligi kuu, atakwenda nacho ligi daraja la kwanza ambapo huko kuna changamoto kubwa zaidi na ndipo atakapodhihirisha ahadi yake ya kubaki St James’ Park.

Benitez alikubali kusaini mkataba wa miaka mitatu wa kukinoa kikosi cha Newcastle Utd mapema mwezi uliopita, na anaamini alichokiafiki kitakuwa mustakabali mzuri kwake kwa maisha ya baadae klabuni hapo.

Kwa sasa Newcastle Utd imesaliwa na michezo sita kabla ya msimu wa 2015-16 haujafikia kikomo, na italazimika kushinda michezo yote ili kujiweka katika mazingira ya kusalia ligi kuu msimu wa 2016-17, huku wakiziombea mabaya klabu zilizo katika vita ya kuporomoka daraja.

Newcastle Utd wamesaliwa na mchezo dhidi ya Swansea City (16 April), Manchester City (April 19), Liverpool (April 23), Crystal Palace (April 30), Aston Villa    (May 07) na Tottenham Hotspur (May 15).

Siri Ya Athumani Iddi Chuji, Jerry Tegete Kukaa Benchi Yafuchuka
Ommy Dimpoz ahamia kwenye kilimo