Sababu za kocha wa Mwadui FC Jamuhuri Kiwelu Julio kushindwa kuwatumia kiungo mkabaji Athumani Idd ‘Chuji’ na mshambuliaji Jerry Tegete, zimefahamika.

Mwadui FC juzi walikabiliwa na mchezo wa kiporo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya mabingwa watetezi Young Africans uliochezwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam, na wachimba madini ya almasi kukubali kufungwa mabao mawili kwa moja.

Taarifa ambazo zimetolewa na matu ambaye alikuwepo wakati wa majadilino ya wachezaji hao kucheza ama kutokucheza mchezo huo, zinaeleza kwamba kikwazo kikubwa kilitokana na Chuji pamoja na Tegete kuwahi kuitumikia Young Africans hivyo walihofiwa huenda wangecheza chini ya kiwango.

Kiungo mkabaji  Athumani Idd ‘Chuji’ na mshambuliaji Jerry Tegete Walipokua akiitumikia Young Africans

 “Chuji na Tegete waliwekwa benchi makusudi na hawakua tatizo lolote, kikubwa ni viongozi walihofia kuwa wangecheza chini ya kiwango kwa kuwa wanakutana na timu yao ya zamani,” alisema mtu huyo ambaye hakutaka jina lake kuanikwa hadharani.

Hata hivyo walipotafutwa wachezaji hao kuzungumzia hilo kwa upande wa Chuji alisema: “Kama unavyojua Anko, mimi nimetokea Yanga kabla ya kuja kuichezea Mwadui, hivyo hiyo sababu inahusika kwa kuwa nipo fiti, kama ningekuwa nina matatizo, basi hata benchi nisingekaa.”

Tegete yeye alisema: “Si unajua tena haya masuala ya soka, kikubwa ninachokiona mimi sikupangwa na kujikuta nakakaa benchi sababu kuwa niliwahi kuichezea Yanga na ndicho kilichoniponza.”

UEFA: Man City Kupambana Na Mabingwa Wa Kihistoria
Rafael Benitez: Nitakua Na Newcastle Utd Popote Itakapokwenda