Rais wa Italia, Sergio Mattarella amesema hatokubali hatua ya kujiuzulu kwa Waziri Mkuu wake Mario Draghi.
Waziri Mkuu, Draghi alisema angejiuzulu baada ya vuguvugu la nyota tano ili kuondoa uungaji wake mkono kwa Serikali.
Draghi alinusurika katika kura ya imani iliyopigwa katika Bunge la Italia kwa kushinda kura 172-39.
Wabunge wa vuguvugu la nyota tano, walikataa kushiriki kura hiyo wakieleza upinzani dhidi ya baadhi ya vipengele vya mpango wa euro bilioni 26 wa kutuliza bei za nishati unazidi kupaa.
Draghi alikuwa amesema, hana nia ya kuongoza bila vuguvugu la nyota tano, huku ofisi ya Mattarella ikisema haitakubali kujiuzulu, na kumualika Draghi kujitokeza mbele ya Bunge.
Mkuu huyo wa zamani wa Benki Kuu ya Ulaya, ECB alichaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa sita wa Italia, kwa miaka kumi hadi 2021.
Endapo Draghi atashindwa kuunda Serikali ya muungano, Mattarella huenda akalivunja Bunge na kuitisha uchaguzi mpya Septemba, 2022.