Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amempongeza DJ maarufu nchini humo, Black Coffee kwa kushinda tuzo za BET katika kipengele cha ‘Best International Act: Africa’  wikendi iliyopita, ambacho wengi walidhani kingeenda kwa Diamond au Wizkid kutokana na ukubwa wao hivi sasa.

Rais Zuma ametoa tamko rasmi kwa vyombo vya habari maalum kwa ajili ya Black Coffee ambaye ameibuka kuwa msanii wa kwanza wa muziki nchini Afrika Kusini kushinda tuzo hiyo.

“DJ Black Coffee anaendelea kuwahamasisha vijana wengi kwa mafanikio yake na hivi sasa amekuwa kitu kikubwa chetu kikubwa kimataifa katika kiwanda cha muziki, kama mfano wa vipaji vya vijana wa Afrika Kusini. Taifa letu linajivunia kuwa naye na mafanikio yake. Tunampongeza kwa moyo mkunjufu,” ilisomeka taarifa ya Rais Zuma.

DJ Coffee ambaye anafanya kazi kwa kutumia mkono mmoja naye alijibu kupitia mtandao wa Tweeter akiwashukuhuru wote kwa kwa kumuunga mkono. Alisema tangu mwaka jana amekuwa akifanya matamasha ndani na nje ya nchi yake na hivi sasa ameyaona matokeo.

50 Cent akamatwa kwa kutoa 'tusi' kwenye mji wa wastaarabu
Mafuriko yasababisha vifo vya watu 24 Marekani