Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” Athuman Juma “Chama” maarufu kama Jogoo aliyefariki usiku wa kuamkia leo Januari 8, 2018 kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili.
 
Katika salamu hizo za rambirambi Rais Karia amesema ni mshtuko mkubwa kumpoteza mchezaji huyo wa zamani na ametoa pole kwa familia yake,ndugu jamaa na marafiki.
 
Rais Karia amesema TFF inatoa rambirambi kwa familia ya marehemu kutokana na msiba huo. 
 
“Ni masikitiko makubwa kumpoteza Chama ambaye alilitumikia taifa naungana kumuombea marehemu na ninatoa pole kwa familia yake,wana familia ya mpira wa miguu ,ndugu na jamaa zake wa karibu pamoja na marafiki,Mungu aiweke mahala pema peponi roho ya Marehemu Athuman Juma Chama .Amina. Inna Lillah wa Innalillah Rajaun.”
 
Enzi za Uhai wake Marehemu Chama pamoja na kuichezea timu ya Taifa katika ngazi ya klabu alicheza kwenye vilabu vya Pamba na Yanga.

Gigy Money atoa chozi Basata
Chuo cha IFM mabingwa ligi ya vyuo