Baada ya kauli ya Rais Magufuli kutoa onyo kwa wizara husika kushughulikia wasanii wanaoimba matusi na wanaovaa nusu utupu, Naibu Waziri wa Sanaa na Michezo Juliana Shonza aliwaita baadhi ya wasanii ofisini kwake akiwemo Gigy Money na wengine kuwafungia kazi zao kwa takribani miezi 6.

Mapema leo hii Gigy Money ameripoti katika ofisi za Basata kufuatia agizo alilopewa na Naibu Waziri Shonza kuwa afike ofisini kwake.

Ambapo Gigy aliongea na waandishi wa habari kwa masikitiko makubwa akiilaumu Serikali na kusema hakuna uhuru wa mtu kufanya mambo yake.

‘’Hakuna freedom tena, hata mtu anakujudge picha ya machi January mwaka jana,  wananiambia tangu nimekuwa video vixin inabidi nijtambulishe na basata’’ amesema Gigy.

Hata hivyo ameeleza kuwa Basata hawamtambui kama ni msanii kwa kuwa hajajisajili.

Gigy anaamini hajafanya kosa kwani amesema ana miaka miwili haja piga picha ya utupu.

‘’Kabla ya mheshimiwa rais kutoa kauli ya utupu mi nilikuwa nimeshaacha’’ amesema Gigy.

Aidha, Gigy amesema kuitwa kwake na waziri sio kwa sababu ya wimbo wa Papa bali anahisi ni yeye ndio mwenye matatizo kwani amesema wapo wasanii ambao wameimba nyimbo zenye tungo tata na hawajachukuliwa hatua.

Amesema hajakiuka kauli ya Serikali kama ambavyo mitandaoni wamedai kwani anaamini hakuna mtu anayeweza kupingana au kushindana na serikali.

Aveva kuhamishiwa Muhimbili
Rais Karia atuma salamu za rambirambi