Rais John Magufuli leo amefanya ziara ya ghafla katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa lengo la kujionea uhalisia wa huduma inayotolewa.

Kama ilivyokuwa alipofanya ziara ya kushtukiza katika Wizara ya Fedha wiki iliyopita, Rais Magufuli alikutana na viongozi wa hospitali hiyo na kuongozana nao katika maeneo ambayo aliyachagua yeye.

Rais Mafuguli amesema kuwa ameamua kufanya ziara hiyo ya kushtukiza kwa lengo la kujionea changamoto zinazowakabili wananchi wakati wanaopata huduma za matibabu katika hospitali hiyo.

Moja kati ya changamoto ambazo alikutana nazo ni pamoja na kuambiwa kuwa baadhi ya mashine za kuchukulia vipimo zilikuwa hazifanyi kazi kwa kipindi cha zaidi ya miezi miwili wakati katika hospitali binafsi mashine hizo zimekuwa zikifanya kazi.

Rais Magufuli ambaye alishangiliwa na wagonjwa baada ya kufika katika hospitali hiyo aliagiza watendaji katika hospitali hiyo kuhakikisha wanatatua tatizo la mashine kutofanya kazi kwakuwa hakupewa sababu msingi zinazopelekea tatizo hilo ili hali zinafanya kazi katika hospitali binafsi.

Aliweza kutembelea wodi ya wazazi pamoja na wodi za watu waliopata ajali ya vyombo mbalimbali vya moto na kujionea changamoto inayowakabili.

Kabla ya kuelekea katika hospitali hiyo ya Taifa, Rais Magufuli alipita katika Hospitali ya Agha Khan kumjulia hali Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Bi. Hellen Kijo Bisimba (pichani) anayepata matibabu katika hospitali hiyo baada ya kupata ajali ya gari katika makutano ya Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es Salaam.

Chelsea Yaangalia Uwezekano Kwa Diego Pablo Simeone
Mashabiki Wa Spurs Walipa Kisasi Emirates Stadium