Serikali ya Botswana, imetoa waranti wa kukamatwa kwa Rais wa zamani wa nchi hiyo, Ian Khama akikabiliwa na mashtaka 14 ya uhalifu ikiwemo kumiliki silaha kinyume cha sheria na utakatishaji wa fedha.

Mara baada ya kupata taarifa hizo, Khama ambaye inasemekana kuwa yupo nchini Afrika Kusini amekanusha mashtaka dhidi yake, akisema ni ya uongo na kwamba yamechagizwa na masuala ya kisiasa.

Rais mstaafu wa Botswana, Ian Khama. Picha ya Daily Maverick.

Khama ambaye alijiuzulu mwaka 2018 baada ya kuhudumu kwa kipindi cha miaka 10, alikosana na mrithi wake, Mokgweetsi Masisi, ambaye amemshutumu kwa kutawala kimabavu.

Hata hivyo, Aprili 2022 Khama alidai anajihisi yuko salama akiwa Afrika Kusini na huenda kamwe asirejee Botswana, huku akikanusha madai ya kuukimbia mkono wa sheria na inaarifiwa kuwa iwapo Mahakama itamkuta na hatua anaweza tumikia kifungo cha  miaka 10 gerezani.

Papa Benedict XVI 95 amefariki dunia
Waandishi wa Habari 1,700 wauawa duniani