Rais wa Urusi, Vladimir Putin ametumia maneno machafu kuishambulia Uturuki kutokana na tukio la kuiangusha ndege yake ya kivita.

Akizungumza katika kikao na waandishi wa habari ambacho hufanyika mara moja kila mwaka, Putin alidai kuwa Uturuki imeilamba Marekani ‘Pahala Pabaya (lugha chafu imefichwa)’ na kuendelea kusisitiza kuwa watajuta.

Katika hatua nyingine, rais Putin alimsifia Donald Trump, anayewania kuchaguliwa na chama chake cha Republican kugombea urais wa Marekani ambaye amekuwa na maneno yanayozua utata mwingi.

Rais Putin alidai kuwa Trump ni mgombea mwenye akili nyingi na kwamba ana kipaji cha hali ya juu.

Baada ya kumwagiwa sifa na rais Putin, Trump naye alijibu kwa kumshukuru akidai ni heshima kubwa kwake.

“Ni heshima kubwa sana kusifiwa na mtu ambaye anaheshimiwa sana ndani ya taifa lake na nje ya taifa lake,” alisema Trump.

Umoja Wa Afrika Kutuma Wanajeshi 5000 Burundi
CAG Adaiwa 'Kuibipu' Nyundo ya Magufuli, Akiuka Agizo Lake