Muungano wa Afrika (AU) umeeleza mpango wa kutuma wanajeshi 5000 wa kulinda amani nchini Burundi kufuatia machafuko yanayokadiriwa kusababisha vifo vya watu zaidi ya 400.

Machafuko na mauaji hayo yalianza baada ya rais Pierre Nkurunzinza kutangaza mpango wa kugombea urais kwa muhula wa tatu kinyume na katiba ya nchi hiyo.

Mpango huo wa AU umeamuliwa katika mkutano wa nchi wanachama wa umoja huo uliofanyika Alhamisi wiki hii jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Taarifa kutoka katika kikao hicho zimeeleza kuwa huenda kwa mara ya kwanza AU ikatumia kifungu kilichoko kwenye katiba ya Umoja huo kwa kupeleka majeshi hayo nchini humo bila kibali cha nchi mwenyeji.

 

 

Nape aeleza jinsi ambavyo Radio na TV zitagawana mapato yake na Wasanii kuanzia Januari
Rais Putin aitusi Uturuki Mbele ya Waandishi Wa Habari, Amsifia Donald Trump