Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amelezea kwa Wananchi wa Mtwara juhudi mbalimbali zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuwapelekea maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya kielimu, afya, barabara na upanuzi wa Bandari ya Mtwara.

Dkt. Biteko ametoa maelekezo hayo hilo hii leo Novemba 15, 2023 Mkoani Mtwara, wakati alipokagua miradi ya umeme vijijini na kuwasha umeme katika Kata ya Naliendele, eneo la Pachota A na Kijiji cha Nachenjele na kuongeza kuwa upanuzi huo utapelekea usafirishaji wa korosho kufanyika kwa urahisi, mafuta kushushiwa katika bandari hiyo na makaa ya mawe kusafirishwa kutokea Bandari ya Mtwara.

Amesema, kutokana na hatua hiyo, Watendaji wa Serikali wanatakiwa kusimamia ipasavyo fedha za Serikali huku akimuagiza Mkuu wa Mkoa Mtwara, kuwachukulia hatua wale wote wanaorudisha nyuma hatua za maendeleo na kuwaasa wananchi kuungana katika kujiletea maendeleo bila kuangalia itikadi za vyama kama ambavyo Serikali inapeleka miradi ya maendeleo  kwenye maeneo yote.

Akiwa katika Kijiji cha Nachenjele, Dkt. Biteko pia ameagiza Shule ya Msingi na Sekondari katika Kijiji hicho kupelekewa umeme na pia ametoa Kompyuta tano kwa shule ya sekondari na tano kwa shule ya msingi.

Awali, Mkurugenzi wa Umeme Vijijini kutoka REA, Jones Olotu alimweleza Naibu Waziri Mkuu kuwa, Mkoa wa Mtwara umetengewa shilingi bilioni 170 kwa ajili ya kusambaza umeme vijijini na kwamba katika vijiji 785 vya mkoa huo, Vijiji 401 bado havina umeme lakini wakandarasi kampuni ya Derm, Central na Namis wanaendelea kusambaza umeme kwenye Vijiji vilivyosalia.

Ametaja miradi inayoendelea kutekelezwa mkoani humo kuwa ni REA Awamu ya Tatu, Mzunguko wa Pili (REA III Round II), Mradi wa kusambaza umeme katika maeneo ya pembezoni mwa miji (Vijiji-Miji) (Peri-Urban III),  Mradi wa Kupeleka umeme kwenye migodi midogo na maeneo ya kilimo, Mradi wa Kupeleka umeme kwenye Vituo vya Afya na Pampu za Maji pamoja na Mradi wa ujazilizi (Densification 2C).

Steven Gerrard amuwashia moto Al-Kuwaykibi
Jawadu apongeza usimamizi miradi kwa ufanisi, ubora