Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amepokea tuzo ya Babacar Ndiaye (2022), Accra nchini Ghana.

Tuzo hiyo imetolewa kwa mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita katika ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji ambayo hutolewa kwa Mkuu wa nchi iliyofanya vizuri.

Rais Samia amesema anajisikia faraja kwa kuwa Rais wa kwanza mwanamke barani Afrika kupokea tuzo hiyo kwani ni heshima kwake na heshima kwa kile anachokifanya katika nchi yake.

Aidha, ameelezea suala la utekelezaji wa miundombinu ni mchakato endelevu ambao umeanza tangu awamu ya kwanza ya muasisi wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere lakini lilishika hatamu zaidi katika awamu ya nne ya utawala wa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ambao uliendelea hadi kufikia katika awamu yake.

Amesisititiza kuwa ili Bara la Afrika liweze kujikomboa kiuchumia miundombinu ni jambo mtambuka na lazima lipewe kipaumbele ili liweze kusaidia kukuza uchumi wa Afrika.

Rais Samia amebainisha kuwa 60% ya ardhi iliyopo Afrika inafaa kwa kilimo, mbali na rasilimali nyingine zilizopo kama vile madini pamoja na utalii amesema kuwa ili vitu hivi viweze kuwa na tija miundombinu mizuri lazima iwepo.

Kizimbani kwa wizi wa dawa za saratani
Dkt. Mpango asisitiza ushirikiano katika kuwezesha tafiti za ndani