Timu ya Yanga na Simba leo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam zitachuana vikali dhidi ya mchezo wa ligi kuu Tanzania bara, ambapo mpaka sasa timu ya Simba inaongoza na endapo itashinda katika mechi hii itakuwa na nafasi kubwa ya kuwa mshindi wa ligi hii.

Aidha Timu ya Yanga na Simba tayari wamechuana takribani katika michezo 100, ambapo kwa idadi hiyo ya michezo, Yanga wameweza kuwashinda Simba kwa mechi 38, huku Simba wakiwa wamewashinda yanga kwa mechi 27, na timu hizo zimewahi kutoka droo kwa mechi 35.

Na katika michezo hiyo Yanga imeweza kushinda magoli 105 huku Simba ikiwa imeshinda magoli 94.

Rekodi hiyo itabadilishwa leo ambapo tayari vikosi vya Simba na Yanga vitakavyoingia dimbani kuchuana vimekwisha pangwa, ambapo kwa Simba wachezaji watakaoingia uwanjani ni;

Manyika Peter, William Lucian, Mohamed Husseni, Hassan Shaka, Joseph Owino, Jonas Mkude, Haruna Chanongo, Said Ndemla, Elias Maguri, Amri Kiemba na Emanueli Okwi.

Huku kikosi cha Yanga wachezaji wake wakiwa, Deogratius Munisi “Dida” Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub “Cannavaro” Kelvin Yondani, Mbuyu Twite, Hassan Dilunga, Haruna Niyonzima, Genilson Santos “Jaja”, Mrisho Ngasa, Andrey Coutinho.

Askari polisi wafungwa jela kwa kushiriki maandamano
Video: Darasa aachia ngoma yake mpya ''Kumbe''

Comments

comments