Mwanamziki mkongwe sana nchini Marekani anayefanya vizuri katika fani hiyo duniani, Robyn Rihanna Fenty anayejulikana kama ‘Rihanna’, tukiwa tunaelekea mwezi wa pili wenye sikukuu ya wapendanao iliyopo tar 14 Februari kila mwaka, ni sikukuu ya mtakatifu Valentine ambapo  katika kunogesha upendo Rihanna ameamua kuwapa zawadi warembo Duniani

Muimbaji huyo ameachia manukato (perfume) yake yanayojulikana kama ‘Kiss by Rihanna’ ikiwa ni mwendelezo wa aina ya tatu ya manukato hayo.

Kupitia mtandao wa Instagram, mrembo huyo ameweka picha ya manukato hayo na kuandika, “With Valentines Day right around the corner I got something special for my ladies!! The 3rd part of the “RiRi” trilogy #KISS is finally here…. available at @macys and online at Macys.com
#KISSbyRihanna.”  (Sikukuu ya wapendanao inakaribia nina kitu cha tofauti kwa warembo wangu, ni toleo la tatu la ”RiRi” trilogy #KISS sasa ipo tayari na inapatikana @macys na mtandaoni Macys.com.#KISSbyRihanna.”).

Gharama za manukato hayo hutofautiana na ujazo ambapo manukato yenye ujazo wa chini kugharimu   dola 30.38 ambayo ni sawa na shillingi 67,838.2362 za kitanzania.

Nje ya muziki Rihanna amekuwa akiingiza fedha nyingi katika tasnia ya mitindo.

 

Tobias Kifaru: Simba Hawatoki Jamhuri
Mbowe: Chadema tunachezewa rafu za kisiasa