Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kupitia kitengo cha Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) kimetoa matokeo ya uchunguzi wa vifo vya samaki wenye kilogramu 156, lililotokea Julai 21, 2021 katika eneo la ufukwe wa AghaKhan Jijini Dar es Salaam ambapo walichukua sampuli za samaki kwaajili ya uchunguzi wa kimaabara.

Ripoti inasema kuwa aina tisa za samaki zilitambuliwa ambazo ni kui, mkizi, janja, tambanji, chaa, kuku bahari, kolekole pandu, kaa, kambamiti na kambakochi, huku samaki jamii ya kui ilichukua sehemu kubwa ya samaki hao kwa asilimia 36 ikifuatiwa na jamii ya mkizi iliyokuwa na asilimia 29 samaki hawa hupatikana kwenye kina kifupi cha maji.

Aidha wengi wa samaki hao walikuwa wachanga Sehemu kubwa ya matumbo ya samaki hayakuwa na chakula, ingawaje aina tatu za samaki kui, mkizi na tambanji walikutwa na dagaa, kaa na uduvi katika matumbo yao.

Samaki waliochunguzwa walikuwa na hali nzuri, ngozi haikutatuka rangi angavu, macho yao yalionekana meusi, angavu, mapezi yalikuwa angavu bila utelezi, nyama zao pia zilikuwa imara wala hakukuwa na harufu mbaya hali ambayo inaondoa uwezekano kuwa vifo hivyo vilitokana na sumu au vilipuzi , ingawa samaki wengi walionekana kuwa na midomo wazi kuashiria kuwa walikosa hewa au walikufa wakitafuta hewa.

Hata hivyo Uchunguzi wa sampuli za maji yaliyochukuliwa katika eneo haukubaini vimeamaji vinavyohusishwa na sumu Mf. Kundi la Microcystis, dianoflagelates, pseudonitchia, na Gambierdiscus spp.

Aidha Maafisa uvuvi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam waliteketeza samaki waliobaki kwaajili ya usalama wa wananchi.

Sambamba na hayo yote vifo vya samaki havikutokana na uwepo wa sumu ya aina yoyote ile kwenye maji eneo la tukio, Kutokana na samaki wengi kuwa na midomo wazi na wengine kuwa na matamvua wazi, uwezekano ni mkubwa kuwa samaki hao walikufa kwa kukosa hewa ya oksijeni.

Kagame CUP: Azam FC kuanza na Tusker, Yanga na Express
Biashara United Mara kujitosa Msimbazi