Rais wa kwanza wa Zimbabwe ambaye ni muasisi na Baba wa Taifa hilo, Robert Mugabe amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95.

Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa amethibitisha kifo cha Mugabe akieleza jinsi alivyoguswa na kuondokewa na mpigania uhuru wa Taifa hilo.

“Kwa majonzi makubwa, natangaza kifo cha Muasisi na Baba wa Taifa la Zimbabwe, Robert Mugabe,” Rais Mnangagwa ameandika kupitia akaunti yake ya Twitter.

“Mugabe alikuwa alama ya ukombozi. Mpigania uhuru wa Afrika aliyejitolea maisha yake kwa ajili ya kuwainua watu. Mchango wake kwa Taifa hili na Bara hili hautasahaulika. Roho yake na ipumzike kwa amani,” ameongeza.

Mugabe alikuwa anasumbuliwa na maradhi ambayo hayakuwahi kuwekwa wazi. Alikuwa akipatiwa matibabu nchini Singapore mara kadhaa, lakini alipatiwa matibabu mfululizo nchini humo tangu Aprili mwaka huu.

Rais wa Zimbabwe aliliambia Taifa hilo kuwa Mugabe alikuwa anasumbuliwa na maradhi pamoja na uzee.

Alikuwa Rais wa Zimbabwe tangu mwaka 1980 hadi mwaka 2017 alipolazimika kujiuzulu.

Rais Mugabe akipiga kura kumchagua Rais wa Zimbabwe, mwaka 2018.

Waziri Mkuu wa Sudan atangaza baraza la Mawaziri
Mke wa Rais wa zamani ahukumiwa kwenda jela miaka 58