Rais wa Ufilipino, Rodrigo Duterte amekiri kuwa alipokuwa kijana alishawahi kufanya mauaji kwa kutumia kisu baada ya kumchoma kijana mmoja aliyekuwa akimtazama sana bila sababu ya msingi.

Ameyasema hayo alipokuwa akiwahutubia raia wa Ufilipino wanaoishi katika mji wa Da Nang nchini Vietnam ambako anahudhuria mkutano mkuu wa viongozi wa nchi za Asia na Pasifiki.

Kiongozi huyo wa Ufilipino anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa Apec pamoja na viongozi wengine akiwemo Rais wa Marekani,Donald Trump kwaajili ya kujadili masuala mbalimbali yahusuyo maendeleo.

“Nikiwa na miaka 16, nilimuua mtu kwa kumchoma na kisu, kwasababu alikuwa akinitizama bila sababu yeyote ya msingi, ndipo nikaamua kumchoma kisu,”amesema Rais Durtete

Aidha, baada ya muda mfupi msemaji wake alisema kuwa tamko la Rais huyo lilikuwa ni utani tu ambao amekuwa akiufanya mara kwa mara pindi anapokutana na kuwahutubia wananchi wa nchi yake.

Hata hivyo, Rais Duterte amekuwa akiwashangaza wengi kuhusu kampeni yake anayohamasisha ya kuwaua watuhumiwa wanaojihusisha biashara ya dawa za kulevya bila kuwafikisha mahakamani.

 

Patrice Evra afukuzwa Marseille
Magazeti ya Tanzania leo Novemba 11, 2017