Shirika la Ndege nchi Rwanda limetangaza kusitisha kwa muda safari zake za ndege za kuelekea na kutoka Entebbe Uganda, kutokana na kuongezeka kwa visa vya Covid-19 nchini humo ambapo shirika hilo limesema kufunguliwa kwa safari hizo bado haijajulikana mpaka litakapotolewa tangazo lingine.
Shirika hilo limesema kuwa wateja waliothiriwa ‘na tangazo hilo wanaweza kupanga upya safari na kusafiri baadaye, pale safari hizo zitakaporejeshwa tena au waombe kurejeshewa pesa zao za nauli.
Hata hivyo Rwanda Air inaomba radhi kwa usumbufu uliosababishwa na hatua hiyo.
Uganda imeshuhudia ongezeko la idadi ya watu walioambukizwa virusi vya corona, jambo lililowalazimisha maafisa kuweka sheria inayowataka watu kupunguza shughuli na matembezi yasiyo ya lazima kwa muda wawiki sita.
Zaidi ya watu 750,000 wamepewa chanjo ya corona nchini Uganda kufikia sasa ambapo Nchi ilikuwa imepokea dozi 964,000 za chanjo ya AstraZeneca mnamo mwezi Machi, ambayo inaelekea kuisha.