Klabu ya Leicester City imethibitisha kuwatema mastaa saba baada ya mikataba yao kufika ukomo mwishoni mwa msimu huu 2022/23.

Leicester City imeshuka daraja kutoka kwenye Ligi Kuu England na sasa ipo kwenye mchakato wa kujijenga na kujipanga upya ili wasikae muda mrefu huko kwenye Championship.

Miongoni mwa wachezaji waliochwa ni kiungo wa kimataifa wa Ubelgiji, Youri Tielemans, ambaye amekuwa akihusishwa na klabu kibao za Ligi Kuu England zinazohitaji saini yake.

Mastaa wengine ni Caglar Soyuncu, Daniel Amartey, Nampalys Mendy, Ryan Bertrand, Ayoze Perez na Tete ambao bila ya shaka watasababisha vita kali kutoka kwa klabu nyingine zitakazowania kunasa saini zao.

Soyuncu inaelezwa atatimkia zake Hispania na imeripotiwa amefikia makubaliano ya kujiunga na Atletico Madrid.

Mshindi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Bertrand ataachana na klabu hiyo baada ya kujiunga nayo miaka miwili iliyopita akitokea Southampton.

Tete alijiunga na Leicester City Januari tu hapo hapo kwa dili fupi, lakini sasa atarejea Shakhtar Donetsk, Julai Mosi. Perez ataondoka jumla baada ya kutumikia nusu ya pili ya msimu uliopita kwa mkopo huko Real Betis.

Kwa nyakati zake alizokuwa King Power, alicheza mechi 114 akifunga mabao 15 na kuasisti 12.

Hata hivyo, Leicester City imeamua kubaki na kiungo Hamza Choudhury, ambaye imemwongezea mkataba hadi Juni 2024.

Leicester ilishinda ubingwa wa Ligi Kuu England msimu wa 2015-16.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Juni 8, 2023
Victor Lindelof apeta Manchester United