Kiungo kutoka nchini Mali na Klabu ya Simba SC Sadio Kanoute ameahidi kuendeleza moto katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, baada ya kuisaidia timu yake kutinga Robo Fainali.

Kanoute alifunga mabao mawili kati ya mabao saba yaliyoizamisha Horoya AC Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam Jumamosi (Machi 18), huku Simba SC ikitinga Robo Fainali kwa kufikisha alama 09 kwenye msimamo wa Kundi C, ikitanguliwa na Raja Casablanca ya Morocco.

Kwa kutambua hilo, Kanoute amesema katika mapumziko waliyopewa amehakikisha anakilinda kiwango chake, na baada ya kurejea kambini makocha wake wasipate tabu ya kuanza upya kumuweka fiti.

“Mchezaji anayejua anategemewa kwenye timu lazima atafanya mazoezi yake binafsi bila kusukumwa, hivyo kukaa nje na kambi hakuwezi kuondoa ufiti na kiwango chake.”

“Pia kufika Hatua ya Robo Fainali kwetu ni fursa nyingine ya kupambania hatua nyingine na inatufanya thamani yetu iwe kubwa dhidi ya timu ambazo tunakumbana nazo,” amesema Kanoute mwenye mabao mawili katika Ligi ya Mabingwa.

Kanoute amesema shida sio kufunga mabao hayo bali ni kuhakikisha anatoa mchango kwa kadri awezavyo anapokuwa uwanjani. “Natamani kutoa mchango kadri niwezavyo.”

Wizara kuimarisha uwiano wa kijinsia uhifadhi Wanyamapori
Taarifa Virusi vya Marburg vyaishtua Uganda