Mshambuliaji wa FC Bayern Munich Sadio Mane, amefanya mazoezi akiwa na ‘mpira kwa mara ya kwanza’ katika kipindi cha miezi mitatu, iliyoshuhudia akiuguza majeraha ya mguu.

Mane aliumia siku chache kabla ya kuanza kwa Fainali za Kombe la Dunia mwishoni mwa mwaka 2022, hatua ambayo ilisababisha kuzikosa Fainali hizo zilizounguruma nchini Qatar.

Mshambuliaji huyo kutoka nchini Senegal, leo Jumanne (Januari 31) ameonekana katika viwanja vya maozezi vya FC Bayern Munich akifanya mazoezi ya kupiga mpira chini ya uangalizi wa Benchi la ufundi la Klabu hiyo.

Mazoezi ya Mane yameendelea kuwapa furaha Mashabiki wa Klabu hiyo, ambao wanatamani kumuona akirejea tena Dimbani, ili kuungana na Wachezaji wenzake kuisaidia The Bavarians.

Hata hivyo haijaelezwa kama Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30 ataweza kuuwahi mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya dhidi ya Mabingwa wa Ufaransa Paris Saint Germain, utakaopigwa majuma mawili yajayo jijini Paris.

Afisa wa Polisi afutwa kazi tukio la maauaji ya raia
Kunani? Jukwaa la Papa laporomoka DRC