Meneja wa mwimbaji Diamond platnumz, Sallam SK ametoa utata juu ya uvumi uliokuwa ukienea kuwa kwa sasa ametengana na msanii Diamond na rasmi ameanza kufanya kazi na mwimbaji Harmonize chini ya Konde Music Worldwide.

Uvumi huo, uliotokana na wawili hao kuonekana wakiwa pamoja kwenye show ya msanii Harmonize iliyofanyika majuma mawili yaliyopita visiwani Zanzibar ambapo Sallam amesema yeye na Harmonize hawana mahusiano ya kikazi tangu alipojitoa WCB na kwamba uvumi unaoendelea hauna ukweli.

Harmonize na Sallam SK.

Amesema, “Kusema eti mimi nitoke menejimenti ya wasafi niende Konde Gang hapana, kitu ambacho naweza kufanya naye kazi arudi Wasafi au mimi nifungue Lebo aje asaini kwenye Lebo yangu hivyo ndi vitu viwili vinaweza kutunganisha”

Sallam ameongeza kuwa, “Ikiwa nitafanya naye kazi huko itakuwa nimeshuka daraja, kwa sababu niko kwenye menejimenti ya juu halafu nishuke tena chini?, kwa mimi sasa hivi ninachotakiwa labda niwe kwenye menejimenti ya Universal, Warner Music au lebo nyingine duniani, ndio huko napotaka kwenda” amesema

Mtoto wa miaka sita ajinyonga kwa Chandarua
Mchengerwa 'aongoza tukio' utolewaji wa hundi