Saudi Arabia na Urusi, zikiwa kama viongozi wa shirika la nishati la OPEC Plus, zimekubaliana kukatwa kwa mapipa milioni mbili ya mafuta kwa siku, ikiwa ni jitihada za kuongeza bei na kupinga juhudi za Marekani na Ulaya kuzuia mapato makubwa yanayovunwa Moscow.
Kutokana na mauzo ghafi, upunguzaji huo unawakilisha takriban asilimia 2 ya uzalishaji wa mafuta duniani na ni wa kwanza katika zaidi ya miaka miwili.
Aidha, wachambuzi wa mambio wanasema kutokana na kupunguza pato, OPEC Plus pia ilitaka kutoa tamko kwa masoko ya nishati kuhusu mshikamano wa kundi hilo wakati wa vita vya Ukraine, kwa nia yake ya kuchukua hatua za haraka kutetea bei.
Ikulu ya White House nchini Marekani, iliukosoa uamuzi huo na kuuelezea katika taarifa kama “kutoona mbali,” kwa kuzingatia hali ya uchumi wa ulimwengu.
Bei ya Brent crude, ni kigezo cha kimataifa, ambacho kilishuka wakati wa kiangazi, kupanda zaidi ya asilimia 1.5 baada ya mkutano huo, na kuongeza faida zilizorekodiwa katika siku za hivi karibuni ikiwemo kurudisha bei katika viwango vilivyoonekana mara ya mwisho katikati ya Septemba.
Hata hivyo, hatua ya OPEC inafichua kushindwa kwa diplomasia ya Rais Biden katika majira ya kiangazi na mwanamfalme wa Saudi Arabia, inayoashiria ushawishi mdogo wa Amerika dhidi ya washirika wake wa Ghuba.